19 Machi 2011 - 20:30

ABNA inatuarifu kuwa:Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetangaza kuwa ripoti iliyotolewa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki kuhusu miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia nchini Iran ina malengo ya kisiasa na kwamba haikuwa na jipya.

aarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema kuwa tathmini ya Moscow kuhusu ripoti ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki Yukia Amano juu ya miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia nchini Iran haikuwa na jambo lolote jipya. Russia imesisitiza kuwa ripoti hiyo inakumbusha jinsi ripoti zisizokuwa za kweli za vyombo vya ujasusi zilivyotumiwa kwa ajili ya kupata uungaji mkono wa nchi mbalimbali kwa ajili ya kuishambulia Iraq katika vita ambavyo viliongozwa na Marekani mwaka 2003. Mkurugenzi Mkuu wa wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) Yukia Amano juzi Jumanne alipuuza taarifa za wakaguzi wa wakala huo nchini Iran wanaothibitisha kwamba miradi ya nyuklia hapa nchini haijakengeuka sheria za kimataifa na badala yake ameathiriwa na mashinikizo ya Marekani na Israel na kutoa ripoti dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.